Waziri wa Fedha afanya mazungumzo na uongozi wa Twiga Cement

DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na uongozi wa Twiga Cement ukiongozwa na Meneja Mkuu wake, Bw. Alfonso Velez, Ofisi za Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo pande hizo zimejadili masuala mbalimbali yanayohusu uendelezaji wa uwekezaji wa Kiwanda cha Saruji cha Twiga.
Mhe. Balozi Omar, aliuhakikishia uongozi huo kuwa Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji nchini ili kuimarisha sekta ya viwanda.Kwa upande wake Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Bw. Alfonso Velez, alisema kuwa lengo la kampuni ni kuendelea kukuza uwekezaji nchini ili kukidhi mahitaji ya soko pamoja na kutoa ajira kwa wananchi.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uchambuzi wa Sera Dkt. Remidius Ruhinduka, Kamishna Msaidizi wa Idara ya Uchambuzi wa Sera, Bw. William Mhoja, Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Mcha Hassan Mcha, Kamishna Msaidizi Idara ya Sheria -TRA, Bw. Gabriel Kimweri, Mjumbe wa Bodi wa Twiga cement, Bw. Raymond Mbilinyi na Mkurugenzi wa Fedha wa Twiga Cement, Bw. Simon Renauld, Meneja Biashara Mwandamizi wa Kampuni hiyo, Mhandisi Danford Semwenda na maafisa waandamizi Wizara ya Fedha

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here