Waziri wa Fedha atoa maagizo kwa Shirika la Bima la Taifa (NIC)

DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameliagiza Shirika la Bima la Taifa (NIC) kuandaa mikakati madhubuti ili kuendana na mwelekeo wa mipango ya muda mrefu ya nchi, ambayo inaonesha fursa kubwa za ukuaji wa Uchumi, hususan katika Sekta ya Bima.
Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ametoa maelekezo hayo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), kwa lengo la kujadiliana masuala mbalimbali kuhusu fursa za kuendelea kukuza uchumi wa nchi.

Alisema katika utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050, kuna fursa kubwa za kiuchumi ambapo sekta ya bima inatajwa kuwa miongoni mwa sekta zenye mchango mkubwa katika kuchochea maendeleo, hivyo NIC ni lazima ijipange namna ya kuchangamkia fursa hizo.
"Tuna mipango mikubwa ya nchi, tukiangalia Mpango wa Miaka Mitano na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 ambayo inaonesha fursa za kiuchumi na fursa katika sekta ya bima, NIC kama shirika la umma lazima tujipange kuelekea mipango hiyo kwa sababu kutakuwa na maendeleo ya viwanda, kutakuwa na kanda za viwanda na kanda maalum za viwanda, kilimo na vitu vingine,” alisema Mhe. Balozi Khamis.

Aidha, aliwaagiza kujitangaza na kuongeza kasi ya utoaji wa elimu ya bima kwa wananchi ili waweze kutambua fursa zinazopatikana katika sekta hiyo pamoja na umuhimu wa bima hususan wakati wa majanga.
Kwa upande wake Mkurungezi Mtendaji wa Shirika la Bima la Taifa (NIC), Bw. Kaimu Abdi Mkeyenge, alisema Shirika hilo limekuwa likifanya vizuri katika kutekeleza majukumu yake.
Alisema, wamejipanga kutoa huduma bora nchini kote na kuwekeza zaidi kwenye miradi ya maendeleo kama viwanda, miundombinu na masoko ya mitaji lengo kuu likuwa ni kuongeza mapato ya Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here