Waziri wa Fedha aipongeza Benki ya Stanbic kwa kushirikiana na Serikali kuendeleza sekta ya fedha nchini

DODOMA-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ameipongeza benki ya Stanbic kwa jitihada zake katika kushirikiana na Serikali kuendeleza sekta ya fedha nchini ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Mhe. Balozi Omar, alitoa pongezi hizo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe kutoka Benki hiyo ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake, Bw. Manzi Rwegasira.

Katika mazungumzo yao pande hizo mbili zimejadili masuala mbalimbali yanayohusu uimarishaji wa sekta ya fedha nchini pamoja na kuiwezesha sekta binafsi kushiriki kuchangamkia fursa zilizopo ili kukuza uchumi.
Mhe. Balozi Omar alitoa rai kwa benki hiyo kuichambua Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi ili kubaini maeneo ambayo inaweza kushiriki katika utekelezaji wa miradi ya ubia kati ya Serikali na sekta binafsi.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Stanbic, Bw. Manzi Rwegasira, alishukuru ushirikiano ambao benki hiyo inapata kutoka Serikalini na kuahidi kuwa itaendeleza ushirikiano huo ili kukuza sekta ya fedha nchini.
Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Wizara ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema na maafisa wengine waandamizi kutoka Wizara ya Fedha na Benki ya Stanbic.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here