Tume ya Uchunguzi wa Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025 jana Januari 29, 2026 imekutana na Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye.
Mkutano huo wa Tume na Sumaye umefanyika katika Ukumbi wa Tanganyika uliopo katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini, Dar es Salaam.
Miongoni mwa yaliyojadiliwa ni pamoja na namna matukio hayo yalivyoanza, athari zake kwa watu, mali na miundombinu pia ushauri wa namna ya kuondokana na matukio hayo.
Tume inaendelea kukutana na makundi mbalimbali wakiwemo waathirika wa Matukio hayo ikiwa na lengo la kupata kiini cha chanzo cha matukio hayo na kuyawasilisha kwa ajili ya hatua zaidi.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo













.jpeg)








