Balozi Njalikai ashiriki ufunguzi wa maonesho ya saba ya Kimataifa ya kahawa na chocolate

ORAN-Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mhe. Iman Njalikai ameshiriki katika sherehe za uzinduzi wa Maonesho ya Saba (7) ya Kimataifa ya Chocolate na Kahawa (CHOCAF) yaliyofanyika jijini Oran Februari 4,2026.
Maonesho hayo yalijumuisha zaidi ya kampuni 100 zinazojihusisha na uchakataji wa kahawa na kakao kutoka ndani na nje ya Algeria na kuhudhuriwa na viongozi wa Serikali pamoja na Mabalozi mbalimbali kutoka nchi zinazozalishaji kahawa kama vile Ethiopia, Uganda, Vietnam na Zimbabwe.
Mhe. Balozi Njalikai alitumia jukwaa hilo kukutana na wadau muhimu wa kahawa na kakao na kampuni za uchakataji wa kahawa na watengenezaji wa bidhaa zaKakao ambapo alielezea fursa zilizopo nchini katika uchakataji wa bidhaa hizo ambazo huzalishwa kwa wingi na kuwakaribisha kufanya biashara na Tanzania.
Aidha, Mhe. Balozi aliwaalika wafanyabiashara wa Algeria kuja nchini kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam (7 7) ili kujionea fursa mbalimbali zilizopo na kutangaza biashara zao katika soko la Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here