Balozi Omar azihimiza Kampuni za Mawasiliano kushiriki utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050

NA BENNY MWAIPAJA

WAZIRI wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amesema kuwa Serikali inatambua mchango mkubwa wa sekta ya mawasiliano katika kukuza uchumi jumuishi wa nchi kupitia mageuzi makubwa ya uchumi wa kidigitali, ulipaji kodi na uboreshaji wa huduma za jamii.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akiongoza kikao chake na Uongozi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo Bw. David Tarimo (hayupo pichani), ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kukuza sekta ya mawasiliano na masuala ya kidigitali katika maendeleo ya Uchumi wa jamii, ambacho kilichofanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mhe. Balozi Omar amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Kampuni ya Simu ya Vodacom ikiongozwa na Mwenyekiti wake wa Bodi, Bw. David Tarimo, katika Ofisi za Hazina-Treasury Square, Jijini Dodoma.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), akizungumza jambo wakati wa Kikao chake na Uongozi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, ulioongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Kampuni hiyo Bw. David Tarimo (hayupo pichani), ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kukuza sekta ya mawasiliano na masuala ya kidigitali katika maendeleo ya uchumi wa jamii, ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Aliishauri sekta ya mawasiliano nchini itumie fursa ya utekelezaji wa Dira ya Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2050 iliyozinduliwa hivi karibuni, kuchangia zaidi maendeleo ya nchi Kupitia matumizi ya teknolojia ambayo itachangia kuongeza ukwasi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb)(kulia), akiagana na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Bw. David Tarimo, baada ya Kikao chake na uongozi wa Kampuni hiyo, kilichojadili masuala mbalimbali ya kukuza sekta ya mawasiliano na masuala ya kidigitali katika maendeleo ya uchumi wa jamii, ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Mhe. Balozi Omar aliahidi kuwa Serikali kwa uopande wake itaendelea kuboresha na kuweka mazingira bora ya uwekezaji ili kuchochea na kukuza mchango wa sekta ya mawasiliano nchini katika kuboresha maisha ya wananchi na kuwawezesha wawekezaji kupata faida.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Bw. David Tarimo (Kulia) akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani) na Kampuni hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kukuza sekta ya mawasiliano na masuala ya kidigitali katika maendeleo ya uchumi wa jamii, ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma. Kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire, akizungumza jambo wakati wa kikao cha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (hayupo pichani) na Kampuni hiyo kilichofanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma, ambapo walijadiliana masuala mbalimbali ya kukuza sekta ya mawasiliano na masuala ya kidigitali katika maendeleo ya Uchumi wa jamii, ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa VODACOM, Bw. David Tarimo, aliishukuru Serikali kwa kuweka mazingira mazuri ya ufanyaji biashara kwa wawekezaji hali iliyoifanya sekta ya mawasiliano kuchangia kodi ya zaidi ya shilingi trilioni 1.1 katika mwaka wa fedha 2024/2025, huku Vodacom ikichangia zaidi ya shilingi bilioni 621 hadi ilipofikia mwezi Machi, 2025.
Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb) (Katikati), Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb) (wa tatu kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Bw. David Tarimo (wa tatu kulia), Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania, Bi. Zuweina Farah (kushoto) na maafisa wengine waandamizi wa kampuni hiyo, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kikao chao kilichojadili masuala mbalimbali ya kukuza sekta ya mawasiliano na masuala ya kidigitali katika maendeleo ya uchumi wa jamii, ambacho kilifanyika katika Ofisi ya Wizara ya Fedha, Treasury Square, jijini Dodoma.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,WF, Dodoma).

Aidha, Bw. Tarimo alieleza kuwa tangu Kampuni yake izinduliwe imewekeza zaidi ya shilingi trilioni 4.5 kwa ajili ya Kujenga miundombinu ya mawasiliano na na mwaka jana 2025 imesaidia jamii zaidi ya shilingi bilioni 3.7 kwa kufadhili miradi mbalimbali ikiwemo sekta za afya, elimu, mazingira na kuwawezesha vijana kiuchumi.

Kikao hicho kilihudhuriwa pia na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mhandisi Mshamu Ali Munde (Mb), Kaimu Kamishna wa Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionisia Mjema, Afisa Mtendaji Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Philip Besiimire, Mkurugenzi wa Masuala ya Nje wa Vodacom Tanzania, Bi. Zuweina Farah, na maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha na Vodacom.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here