Benki Kuu za EAC zajifunza mpango wa ununuzi wa dhahabu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

MWANZA-Benki Kuu za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) za Kenya, Uganda, Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC), Burundi, Somalia na Sudani ya Kusini zimetembelea Benki kuu ya Tanzania Tawi la Mwanza kwa lengo kujifunza kuhusu utekelezaji wa mpango wa dhahabu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).Ziara hiyo inafuatia maagizo ya Mkutano wa 28 wa Kamati ya Masuala ya Fedha ya EAC (Monetary Affairs Committee-MAC) uliofanyika mwezi Mei, 2025 ambao uliielekeza BoT kujengea uwezo benki kuu nyingine katika ukanda wa EAC kuhusu utekelezaji wa mpango wa ununuzi na uuzwaji wa dhahabu ambao BoT imepiga hatua kubwa tangu kuanzishwa kwake Oktoba,2024.

Akizungumza katika kikao cha ufunguzi wa ziara hiyo mkuu wa Chuo cha Benki Kuu,Dkt. Nicas Yabu, alisema kuwa mpango wa ununuzi wa dhahabu unasadia kutofautisha vyanzo vya akiba ya fedha za kigeni na kuongeza akiba hiyo.
“Katika zama hizi ambazo uchumi wa dunia unapitia mabadiliko, ni muhimu kutumia rasilimali asilia zilizopo katika ukanda wetu, hususan dhahabu, ili kuboresha na kutofautisha vyanzo vya akiba zetu za fedha za kigeni pamoja na kuongeza kiwango cha akiba tulizonazo,”ameeleza Dkt.Yabu.

Aliongeza kuwa,mivutano ya kisiasa inayotokea ulimwenguni imezilazimu benki kuu nyingi duniani kuongeza akiba zao za dhahabu kupitia ununuzi wa dhahabu.

Dkt.Yabu alieleza kuwa kufika tarehe 12 Februari 2026 BoT imekwisha nunua tani 19.38 za dhahabu zenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 3.07.
Katika ziara hiyo iliyoanza tarehe 16 hadi 20 Februari 2026 washiriki walipata fursa ya kutembelea kiwanda cha kusafishia dhahabu cha Mwanza Precious Metals Refinery na kile cha kusafishia madini ya dhahabu cha mkoani Geita.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here