BoT yashiriki IFEM,yauza dola za Marekani milioni 7.00

NA DIRAMAKINI

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeshiriki katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (IFEM) kwa mujibu wa Sera yake ya mwaka 2023 ya ushiriki katika soko hilo.
Katika ushiriki huu, Benki Kuu imeuza Dola za Marekani milioni 7.00 kupitia mnada wa ushindani kwa kiwango cha wastani cha kubadilisha fedha za kigeni cha Shillingi 2,556.96 kwa Dola moja ya Marekani.

Lengo la mnada huu lilikuwa ni kupunguza mabadiliko makubwa ya muda mfupi ya kiwango cha ubadilishaji wa Shilingi ya Tanzania dhidi ya sarafu za kigeni.

Kwa mujibu wa matokeo ya mnada huo, kiasi kilichotangazwa kilikuwa Dola za Marekani milioni 5.00, huku kiasi kilichowasilishwa na washiriki kikifikia Dola milioni 10.75, ishara ya kuongezeka kwa mahitaji katika soko.

Hata hivyo, Benki Kuu ilikubali zabuni zenye thamani ya Dola milioni 7.00.Kiwango cha juu cha ushindani kilifikia Shilingi 2,615.00 kwa Dola moja, wakati kiwango cha chini kilikuwa Shilingi 2,500.00.

Pia, kiwango cha juu kilichokubaliwa kilikuwa Shilingi 2,580.00 na cha chini kilichokubaliwa kilikuwa Shilingi 2,500.00 kwa Dola moja ya Marekani. Jumla ya benki 14 zilishiriki katika mnada huo, ambapo benki 10 zilifanikiwa kushinda zabuni zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here