Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) anayesimamia Utawala na Udhibiti wa Ndani, Dkt. Rahma Salim Mahfoudh, amewasili katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya BoT jijini Dar es Salaam, ambapo amepokelewa na Gavana wa BoT, Bw. Emmanuel Tutuba, pamoja na viongozi waandamizi wa Benki Kuu, tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu yake mapya.



