EWURA yatangaza bei mpya za mafuta kwa mwezi Februari 2026, mafuta yashuka bei

NA DIRAMAKINI

MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta aina ya petroli zitakazotumika hapa nchini kwa mwezi kuanzia leo Februari 4,2026, zikionesha kushuka maradufu kwa bei  ya mafuta yaliyopokelewa bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dkt. James Mwainyekule imebainisha kuwa, bei ya rejareja ya petroli na dizeli imepungua kwa shilingi 90 kwa mafuta yaliyopokelewa Dar es Salaam, 25 kwa Tanga na shilingi 24 kwa bandari ya Mtwara.

Aidha, bei ya mafuta ya taa nayo imepungua kwa shilingi 17, 14 na 93 kwa mafuta yaliyopokelewa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia ikilinganishwa na bei za mwezi Januari 2026.

Hivyo, bei za reja reja za bidhaa za mafuta kwa mwezi huu, zitakuwa shilingi 2,788, 2,849 na 2881 kwa Dar es Salaam, Tanga na Mtwara mtawalia. Na bei ya dizeli, Dar es Salaam ni shilingi 2,701, Tanga 2,762 na Mtwara 2,807 huku bei ya mafuta ya taa kwa Dar es Salaam ikiwa ni shilingi 2,881, Tanga 2794 na Mtwara 2,838.

Aidha, kwa mwezi Februari 2026, gharama za kuagiza mafuta katika Bandari ya Dar es Salaam ziliongezeka kwa wastani 1.88% kwa mafuta ya petroli na 1.65% kwa mafuta ya taa na kupungua kwa wastani wa 5.10% kwa mafuta ya dizeli.

Kwa bandari ya Tanga zimepungua kwa 1.62% kwa petroli na dizeli; huku bandari ya Mtwara zikipungu kwa 9.24% kwa mafuta ya petroli. Vilevile, wastani wa gharama za kubadilisha fedha za kigeni umeongezeka kwa 1.86%.

EWURA inawahimiza wauzaji wa mafuta nchini kutoa stakabadhi za mauzo kwa wanunuzi zinazoonesha jina la kituo, tarehe, aina ya mafuta yaliyonunuliwa na bei kwa lita. Aidha,vituo vyote vya mafuta nchini vichapishe bei za bidhaa za mafuta katika mabango yanayoonekana bayana kwani kutokufanya hivyo ni kosa na atakayekiuka atapata adhabu kali kwa mujibu wa sheria.

Tazama bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petroli kuanzia leo Jumatano, Februari 4,2026;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here