Kamati ya Bajeti yaipongeza BoT kwa utekelezaji wa majukumu na usimamizi bora wa Sekta ya Fedha

DODOMA-Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba, ametoa wasilisho kuhusu muundo, majukumu na utekelezaji wa kazi za Benki Kuu kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti. Wasilisho hilo pia lilihusisha majibu ya hoja na maswali mbalimbali yaliyoulizwa na wajumbe wa kamati hiyo.
Wasilisho hilo limetolewa leo Jumanne, Februari 10, 2026, katika Ukumbi wa Pius Msekwa, Bungeni jijini Dodoma ambapo Gavana Tutuba aliambatana na Wakurugenzi pamoja na baadhi ya Mameneja kutoka BoT.
Lengo la wasilisho hilo lilikuwa ni kuwajengea uelewa wajumbe wa Kamati ya Bajeti kuhusu namna Benki Kuu inavyotekeleza majukumu yake ya msingi, ikiwemo usimamizi wa sera ya fedha, akiba ya taifa pamoja na udhibiti wa watoa huduma katika sekta ya fedha.

Baada ya wasilisho la Gavana Tutuba, Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, ambaye pia ni Mbunge wa Maswa Magharibi, Mhe. Mashimba Ndaki, aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania kwa utekelezaji thabiti wa majukumu yake na uangalizi wa sekta ya fedha kwa ujumla.
Aidha, aliipongeza BoT kwa hatua ilizochukua kukabiliana na changamoto ya uhaba wa dola za Marekani iliyokuwepo awali, hali iliyosaidia kurejesha utulivu katika soko la fedha za kigeni.

Kikao hicho kimefanyika ikiwa ni siku 28 tangu kamati za kudumu za Bunge ziundwe na kuchagua viongozi wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here