Kocha Gamondi rasmi kuinoa Taifa Stars

DAR-Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Paul Makonda, ameweka wazi kuwa, Kocha Miguel Gamondi amesaini rasmi mkataba wa kuifundisha timu ya Taifa ya soka ya Tanzania (Taifa Stars).
Waziri Makonda amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo Februari 16, 2026, wakati wa Hafla ya Utiaji Saini Mkataba wa Kocha huyo iliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Amesema, Gamondi amestahili mkataba huo baada ya kuonesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya AFCON 2025 iliyofanyika Morocco hivi karibuni na kuingoza Taifa Stars kufika hatua ya 16 ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania akiwa kocha wa muda.
Serikali sasa imeamua kumwajiri rasmi ili aiongoze timu hiyo katika jitihada za kunyakua ubingwa wa AFCON 2027, ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji wa mashindano hayo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here