LATRA yatangaza njia mpya za daladala Dar

DAR-Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) imetangaza njia mpya za mabasi ya abiria pamoja na zile zenye uhitaji wa kuongezewa idadi ya magari, ikiwa ni hatua ya kuboresha upatikanaji wa huduma za usafiri jijini Dar es Salaam.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa Februari 17,2026 na LATRA ambapo imefafanua kuwa, hatua hiyo inalenga kupunguza changamoto za usafiri kwa wananchi kwa kuongeza upatikanaji wa mabasi katika maeneo yenye mahitaji makubwa.

LATRA imetambulisha njia mpya nane zitakazoanza kuhudumiwa na mabasi yenye ujazo wa kuanzia abiria 25, ambapo kila njia itakuwa na jumla ya magari 25.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,njia hizo ni pamoja na kutoka Videte kwenda Buza Stendi kupitia Mvuti na Kilungule. Njia ya pili ni kutoka Videte kwenda Mbezi Luis kupitia Mvuti, Kivule na Malamba Mawili.

Njia ya tatu ni kutoka Videte kwenda Mbezi Luis kupitia Nyerere, Ulongoni na Malamba Mawili. Njia ya nne ni kutoka Videte kwenda Kivule Hospitali kupitia Mvuti, Msongola na Fremu Kumi.

Njia ya tano ni kutoka Videte kwenda Tabata Segerea kupitia Nyerere na Majumba Sita. Njia ya sita ni kutoka Videte kwenda Tabata Segerea kupitia Mvuti, Kivule na Majumba Sita.

Aidha, njia ya saba ni kutoka Mburahati sokoni kwenda Mloganzila kupitia Maji Chumvi na Morogoro, huku njia ya nane ikiwa ni kutoka Mbezi kwenda Tegeta Nyuki kupitia Msumi na Madale.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here