Jeshi la Polisi mkoani Geita linamshikilia Bahati Bushirika anayetuhumiwa kujihusisha na wizi kwa kutumia dawa za kienyeji kuwafanya waathirika wapate usingizi ili kutekeleza uhalifu.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Kamishina Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SCAP) Safia Jongo ametoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari na kueleza mhusika ni mkazi wa kata ya Nyankumbu.Amesema uchunguzi umebaini mtuhumiwa alijiingiza kwenye matukio ya uhalifu baada ya kuacha uganga wa tiba za asili kwa madai ya kukosa wateja pamoja na kukiuka masharti ya kazi hiyo.
Amesema mtuhumiwa anadaiwa kutumia dawa za asili kuwafanya waathirika wapate usingizi kabla ya kutenda uhalifu ambapo alikamatwa katika oparesheni ya mwezi Februari 2026.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





























