Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu- Kazi, Ajira na Mahusiano Deus Sangu amewataka Mawakala binafsi wa Ajira kuzingatia mwongozo wa uratibu wa ajira za nje ya nchi ili watanazania wengi wanufaike na fursa za ajira zinazozalishwa.
Waziri Sangu ameyasema hayo Dar es Salaam jana Februari 19,2026 wakati alipofanya mkutano na Mawakala binafsi 148 wa ajira za ndani na nje uliolenga kutoa mwelekeo wa Serikali kuhusu uzingatiaji wa uratibu wa kisheria na kimfumo.
“Zamani kulikuwa uholela na ndio maana mmeniletea changamoto ya vishoka, Serikali haitambui uwepo wa hao vishoka.Hivyo tumeanzisha mifumo ya kisheria na ya kitaasisi inayosimamia ajira za ndani na nje ya nchi,” alisisitiza Waziri Sangu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


























