DAR-Askofu Mkuu mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Polycarp Kardinali Pengo amefariki dunia katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa usiku wa kuamkia leo Februari 20, 2026 na Askofu Kuu wa Jimbo hilo,Yude Ruwai'chi.
Amesema, Kardinali Pengo amefarki dunia saa 4:00 usiku wa Februari 19, 2026 ambapo taratibu za mazishi zitatolewa baadaye.

