Magazeti leo Februari 21,2026

Naibu Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile, amesema maendeleo ya mradi wa ukarabati wa Meli ya MV Liemba mkoani Kigoma yanaridhisha na utekelezaji wake umefikia zaidi ya asilimia 55.
Kihenzile amesema hayo jana katika ziara ya kukagua miradi ya maendeleo mkoani Kigoma ambapo Naibu waziri huyo ameeleza kuridhishwa na kasi ya ukarabati huo na kusisitiza umuhimu wa meli hiyo katika kuchochea uchumi na kurahisisha usafiri katika Ziwa Tanganyika.

Aidha, Kihenzile amepata fursa ya kutembelea boti ya utafutaji na uokoaji iliyonunuliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania. Alifafanua kuwa boti hiyo itasaidia kuongeza uwezo wa kukabiliana na ajali za majini, matukio ya dharura pamoja na vitendo vya uhalifu katika Ziwa Tanganyika.

Pia,Naibu waziri huyo ameeleza kuwa uwekezaji huo una lengo la kuimarisha usalama wa wasafiri na mali zao, sambamba na kuboresha huduma za usafiri majini, huku akisisiitiza kuwa serikali itaendelea kuwekeza katika miundombinu ya usafiri ili kuhakikisha sekta hiyo inachangia kikamilifu maendeleo ya taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here