Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Morogoro imewataka walipakodi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Morogoro kuanza kuuzoea na kuutumia Mfumo Mpya wa Usimamizi wa Kodi za Ndani wa Kielektroniki (IDRAS), unaolenga kuboresha ukusanyaji na usimamizi wa kodi kwa njia ya kisasa, rahisi na yenye ufanisi zaidi.
Akizungumza na walipakodi na wadau wa kodi mkoani humo Afisa Msimamizi wa Kodi kutoka TRA makao makuu Bw. Ernest Shirima, amesema mfumo wa IDRAS unakwenda kuchukua nafasi ya mifumo mbalimbali inayotumika kwa sasa ndani ya TRA, hatua itakayowezesha kuimarisha utoaji wa huduma za kodi kwa njia ya kidijitali.Bw. Shirima amesema kuwa utekelezaji wa IDRAS utaleta mapinduzi makubwa kwa kuondoa matumizi ya huduma za makaratasi (manual) na kuwezesha shughuli zote zinazohusiana na usimamizi wa kodi za ndani kufanyika kwa njia ya kielektroniki.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo








