Mbolea za Mwani kufungua fursa mpya za kilimo hai Zanzibar na Tanzania Bara

ZANZIBAR-Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata mbolea za mwani katika Wilaya ya Kaskazini Pemba unatajwa kuwa hatua muhimu katika kufungua fursa mpya za kilimo hai, kuongeza tija ya mazao ya mbogamboga, matunda na viungo, pamoja na kuimarisha uchumi wa wakulima Zanzibar na Tanzania Bara.
Akizungumza leo Februari 4, 2026, Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Joel Laurent amesema, Zanzibar ina fursa kubwa ya kuendeleza kilimo kutokana na mwelekeo wake wa uzalishaji wa mbogamboga, matunda na viungo.
Aidha,Laurent amesema TFRA inaamini kuwa kiwanda cha kuchakata mbolea za mwani kitaongeza uzalishaji na ubora wa mazao, huku masoko ya mbolea za organic yakiendelea kukua kwa Tanzania Bara, jambo linaloifanya mbolea ya mwani kuwa na nafasi kubwa ya kibiashara na kukuza kilimo endelevu.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mwani Zanzibar (ZASCO), Mwadini Haji, amesema mradi huo unatarajiwa kuzalisha tani 24,000 za mbolea kwa kutumia mwani mkavu na tani 60,000 kwa kutumia mwani mbichi, hatua itakayoongeza upatikanaji wa mbolea za organic kwa wakulima na kukuza matumizi ya pembejeo rafiki kwa mazingira.

Haji amesema ZASCO inategemewa kuwa mhimili muhimu kwa wakulima kwa kuwapatia mbolea salama na yenye kuongeza ubora wa mazao, sambamba na kuinua thamani ya zao la mwani.
Naye Mkurugenzi wa Masoko wa ZASCO, Kazija Mussa Msheba, amesema baada ya kuanza uzalishaji wa mbolea hizo, kampuni itaanzisha mashamba darasa Zanzibar na Tanzania Bara ili kuwajengea wakulima uelewa wa matumizi sahihi ya mbolea za mwani kwa vitendo na kuongeza tija ya uzalishaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here