Mtumishi wa DAWASA Kibamba ahukumiwa kulipa faini shilingi milioni 1 na kurejesha fedha za rushwa alizopokea shilingi 297,000

DAR-Nsajigwa Dominico Mwaipyana ambaye ni Afisa Msaidizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) Kibamba katika Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam amehukukiwa kulipa faini ya shilingi milioni 1.
Sambamba na kurejesha fedha za rushwa shilingi 297,000 alizopokea ambazo alizipokea kaa mlalamikaji ili arejeshe huduma ya maji aliyokuwa ameisitisha kwa kosa la kujiunganishia kinyume na taratibu (by pass).

Hukumu hiyo imetolewa Februari 17,2026 katika Mahakama ya Wilaya ya Ubungo jijini Dar Es Salaam.

Katika shauri hilo Na. 15649/2025, mshtakiwa Nsajigwa Dominico Mwaipyana alishtakiwa kwa makosa mawili ya kuomba rushwa ya kiasi cha shilingi 300,000 na kupokea kiasi cha shilingi 297,000.

Kosa ambalo ni kinyume na kifungu cha 15(1) (a), 2 na 3(b) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa SURA 329 R.E 2022, kutoka kwa mteja aliyesitishiwa huduma baada ya kujiunganishia maji hayo kinyume na taratibu.

Mshtakiwa alipatikana na hatia kwa makosa yote mawili na kuhukumiwa kilipa faini ya shilingi 500,000 kwa kila kosa au kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela na kurejesha fedha kiasi cha shilingi 297,000 alizopokea.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Ubungo leo Februari 18, 2026 imeeleza kuwa,shauri hili liliendeshwa na wanasheria Anifa Kapinga na Sophia Nyanda.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here