Mwanasheria Mkuu wa Serikali aongoza zoezi la kutoa huduma za kisheria kwa wananchi

DAR-Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mhe. Hamza S. Johari amewaongoza Mawakili wa Serikali kutoa huduma za ushauri wa Kisheria kwa wananchi wakati wa Kliniki ya Sheria bila malipo iliyozinduliwa tarehe 16 Februari, 2026 katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Mhe. Johari amemuhudumia mwananchi aliyekuja kupata huduma ya ushauri wa kisheria ambapo alimsikiliza na kumuhudumia Bi. Sarah Mohamed aliyewasilisha malalamiko yake kuhusiana changamoto ya mirathi inayomkabili.
“Tumeyapokea malalamiko yako na mimi pamoja na timu tutayafanyia kazi kwa haraka ili kuweza kutatua changamoto inayokukabili,"amesema Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Katika zoezi hilo la kutoa huduma kwa wananchi Mwanasheria Mkuu wa Serikali aliambatana na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Zainab A. Katimba.
Timu ya Mawakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali imepiga kambi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam kutoa huduma mbalimbali za kisheria bila malipo kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam kuanzia tarehe 16 hadi 22 Februari, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here