Waziri Dkt.Akwilapo ashiriki kikao cha mawaziri wa wizara za kisekta Lushoto mkoani Tanga

TANGA-Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt.Leonard Akwilapo leo Februari 16, 2026 ameshiriki kikao cha Mawaziri wa Wizara za Kisekta kinachojadili changamoto za sekta ya ardhi zilizojitokeza katika ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Dkt Mwigulu Nchemba mkoani Tanga.
Kikao hicho ni utekelezaji wa maelekezo ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt.Mwigulu Nchemba kuwataka mawaziri hao kukutana haraka na kutafuta suluhu za changamoto zilizojitokeza wakati wa ziara yake mkoani Tanga.
Kikao hicho kinashirikisha Mawaziri kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Maliasili na Utalii, Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Kilimo, Maji, Uvuvi na Migugo pamoja na Wizara ya Fedha.

Baadhi ya changamoto zilizoibuliwa wakati wa ziara ya Waziri Mkuu ni malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Msomera, Handeni Tanga kudai ardhi yao kuchukuliwa pamoja na mgogoro wa mpaka kati ya wilaya ya Kiteto mkoani Manyara na Kilindi mkoa wa Tanga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here