RUKWA-Koplo wa Polisi Kassim Rashid kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa amewaonya na kuwaelimisha madereva wa magari ya biashara pamoja na watu binafsi wanaoendesha magari makubwa na madogo kuhusu madhara ya kutumia vilevi vinavyoweza kusababisha kukosa umakini barabarani.
Elimu hiyo imetolewa Februari 1, 2026 wakati Koplo Rashid akiwa katika kituo chake cha ukaguzi akitekeleza majukumu ya kuhakikisha usalama wa watumiaji wa barabara wilayani humo.Madereva wamekumbushwa pia madhara ya kuendesha mwendo kasi, huku wakisisitizwa kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kupunguza ajali na kulinda maisha yao pamoja na wananchi wengine.



