Naibu Katibu Mkuu mpya wa Wizara ya Fedha,Nsubili Joshua alakiwa ofisi ndogo za wizara Dar

DAR-Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, atakayekuwa anashughulikia masuala ya Utawala (Huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua amepokelewa na viongozi na baadhi ya watumishi wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushika wadhifa huo.
Baada ya kuwasili, Bw.Joshua alilakiwa na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, ambaye pia ni Naibu Waziri anayesimamia Sera za Uchumi, Bw. Elijah Mwandumbya, na baadae kukaribishwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), ambaye alifanya kikao kifupi na Naibu Katibu Mkuu mpya, pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Ofisi Ndogo ya Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Bw. Nsubuli Joshua, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu-Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Omolo, ambaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mpya ya Vijana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here