Msajili wa Hazina aikaribisha Jeune Afrique Media Group kuangazia fursa za uwekezaji

DAR-Leo Februari 9,2026,Msajili wa Hazina, Bw. Nehemiah Mchechu, amekutana na kufanya mazungumzo na Bw.Frederic Van de vyver Mkuu wa Jeune Afrique Media Group, kampuni inayoongoza ya habari ya ki-panafrika yenye makao yake makuu jijini Paris, Ufaransa.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, wamejadiliana ni kwa namna gani wanaweza wakafanya kazi pamoja katika fursa mbalimbali za uwekezaji zilizopo nchini.

Bw. Mchechu amemhakikishia Bw.De vyver kuwa, Tanzania ina mazingira mazuri ya uwekezaji na kwamba atapata ushirikiano wa kutosha.
"Kwa upande wa sekta ya umma utapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Ofisi ya Msajili wa Hazina na kwa upande wa sekta binafsi utapata ushirikiano kutoka kwa CEOrt,” amesema Bw. Mchechu.
Kwa upande wake Bw. De vyver ameeleza dhamira yake ya kuimarisha ushirikiano na Tanzania. "Lazima tutafute namna bora ya kushirikiana,” amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here