ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua CPA Mussa Ali Juma kuwa Kamishna wa Idara ya Usimamizi wa Deni la Taifa.
Kabla ya uteuzi, CPA Juma alikuwa Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Shirika la Taifa la Biashara la Zanzibar (ZSTC).

