Rais Dkt.Samia amuapisha Naibu Katibu Mkuu mpya Wizara ya Fedha

DAR-Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemwapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, atakayekuwa anashughulikia masuala ya Utawala (Huduma za Hazina), Bw. Nsubili Joshua, Ikulu jijini Dar es Salaam.
Uapisho huo umeshuhudiwa na Viongozi wa Wizara ya Fedha, wakiongozwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), Kaimu Katibu Mkuu, Bw. Elijah Mwandumbya, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Lusius Mwenda, na Maafisa wengine waandamizi wa Wizara ya Fedha.
Bw. Nsubuli Joshua, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu-Huduma za Hazina, Bi. Jenifa Omolo, ambaye aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuwa Katibu Mkuu wa Wizara mpya ya Vijana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here