Serikali kufungua fursa za ajira kupitia mikataba mitano

DAR-Serikali Kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi,Ajira na Mahusiano imesaini mikataba mitano ambayo itawawezesha wananchi kupata ajira nje ya nchi.
Hayo yamesemwa Februari 7, 2026 jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu wakati wa Hafla ya Chakula cha Jioni (Gala Dinner) kilichohusisha uzinduzi rasmi wa kipindi cha Imbeju-Bongo Fursa na Jarida la Mapitio ya Vijana lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Biashara na Maendeleo.

“Nilikuwa Falme za Kiarabu nimekutana na Mawaziri wa Kazi kutoka nchi mbalimbali na wote walionyesha nia nzuri na nchi yetu, hadi sasa tumesaini mikataba mitano ambayo iko tayari ya mashirikiano na nchi hizi kwa ajili ya Fursa za Ajira kwa Vijana,”amesema.
Aidha,Mhe. Sangu amesema fursa zilizotajwa kwenye Dira ya Taifa zinapatikana kupitia wizara hiyo na Serikali inafanya mazungumzo ya mwisho kwenye Mikataba 16 ya Ajira kwa ajili ya Watanzania.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa NEDC, Jesse Madauda amesema lengo la Jarida na Kipindi hicho ni kuwatia moyo vijana na kuwafikia wawekezaji ili waone vijana wa Kitanzania wanafanya shughuli za kibunifu na hatua walizofikia ili iwe rahisi kuwafikia wajasiriamali hao.
Awali akizungumza mmoja wa wajasiriamali, Elizabeth Consoli ameishukuru serikali kwa kuwa pamoja na wajasiriamali wavumbuzi na kuonyesha nia ya kuwavusha wajasiriamali hao kutoka hatua moja kwenda hatua nyingine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here