TAKUKURU Mwanza yaokoa shilingi milioni 85+ za malipo ya walimu 77

MWANZA-Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) Mkoa wa Mwanza imefanikiwa kudhibiti fedha kiasi cha Shilingi millioni 85,006,000, fedha ambayo ni madai ya walimu wa shule za sekondari katika Halmashauri ya jiji la Mwanza, madai ambayo yalicheleweshwa kwa zaidi ya miezi sita.
Hayo yamesemwa leo Februari 25,2026 na Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Mha.Abnery Mganga alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kwa lengo la kutoa taarifa kwa umma.

Mafanikio haya ni baada ya TAKUKURU kufanya Uchambuzi wa mfumo na Halmashauri kutekeleza mapendekezo yaliyotolewa na TAKUKURU ambapo imepelekea walimu hao 77 kulipwa stahiki zao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here