Watuhumiwa 73 wakamatwa kwa makosa mbalimbali Manyara

MANYARA-Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limesema limewakamata watuhumiwa 73 kwa tuhuma za makosa mbalimbali ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya, wizi na kukutwa na nyara za serikali kinyume cha sheria
Akizungumza katika kipindi cha Redio cha Mseto wa Leo kinachorushwa na 92.3 FM Manyara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ahmed Makarani Februari 17, 2026, akiwa ameambatana na SSP Mussa Missana Mkuu wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Manyara pamoja na ASP Mohamed Ramadhani Mkuu wa TEHAMA Manyara amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika misako na operesheni zilizofanyika kwa kipindi cha kuanzia Novemba 1, 2025 mpaka Januari 30, 2026 mkoani hapa

Makarani amesema, katika kipindi hicho jumla ya Kilogramu 364 na gramu 700 za dawa za kulevya aina ya Mirungi zilikamatwa na watuhumiwa 17 huku jumla ya kilograms 100.5 za bangi na watuhumiwa wawili wakikamatwa pia

Aidha,katika kipindi hicho lita 389 na mtambo mmoja wa kuchemshia pombe haramu ya gongo ulikamatwa pamoja na watuhumiwa 24

SACP Makarani ameendelea kuiomba jamii kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuzuia matukio hayo yasiendelee katika jamii

Pia ametoa wito kwa wananchi mkoani humo kuacha kujihusisha na matukio ya uhalifu kwani Jeshi la Polisi halitakuwa na muhali kwa mtu au kikundi cha watu watakaobainika kujihusisha na matukio hayo

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here