DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), leo tarehe 25 Februari 2026, amekagua ujenzi wa mradi wa mabweni ya Chuo cha Kodi, kinachomilikiwa na Wizara ya Fedha Kupitia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kilichopo katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam.
Jengo hilo lenye ghorofa saba, lina vyumba 195 vya kulala, kumbi za mikutano, kantini, nyumba ya msimamizi wa jengo, huduma ya wauguzi, afya na mahitaji mengine ya msingi ambapo hadi litakapokamilika litagharimu shilingi bilioni 15.4.
Mhe. Balozi Omar, aliipongeza TRA kwa kuendelea kuboresha mazingira ya utoaji elimu katika Chuo hicho kinachotumika kuwanoa watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, na wanafunzi wengine kutoka ndani na nje ya nchi.










