Waziri wa Fedha ateta na Mabalozi wa Uingereza na Sweden

DAR-Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb), amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza Mhe. Marianne Young pamoja na Balozi wa Sweden nchini Mhe. Charlotta Ozaki Macias katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo hayo, Waziri alisisitiza dhamira ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuendelea kushirikiana na washirika wa maendeleo katika kuimarisha sekta mbalimbali, hususan zile zinazogusa moja kwa moja maisha ya wananchi.
Alibainisha kuwa,ushirikiano wa nchi na nchi ni chachu ya kufanikisha miradi ya maendeleo na kuongeza ustawi wa kijamii na kiuchumi.

Aidha, Mhe. Balozi Omar, alisisitiza kuwa Serikali itaendelea kufanya shughuli zake kwa uwazi na uwajibikaji katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo, huku akiwahakikishia washirika wa maendeleo kuwa Tanzania iko tayari kushirikiana kwa dhati ili kufanikisha malengo ya pamoja.

Kwa upande wao, Mabalozi wa Uingereza na Sweden walieleza kuwa nchi zao zinathamini uhusiano wa muda mrefu na Tanzania na wataendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali za maendeleo.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-Maamry Mwamba, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban, Kamishna Msaidizi, Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha Bw. Melckzedeck Mbise na Wajumbe kutoka Ubalozi wa Uingereza na Sweden.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here