Ayatollah Ali Khamenei auawa kwa shambulio

TEHRAN-Kiongozi Mkuu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Ayatollah Ali Khamenei amedaiwa kufariki dunia kufuatia shambulio kubwa lililotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Marekani na Israel dhidi ya maeneo mbalimbali nchini Iran, ikiwemo makazi yake makuu mjini Tehran.
Hayo ni mujibu wa taarifa mbili muhimu ambazo zimethibitishwa rasmi na vyombo vya habari vya serikali ya Iran pamoja na taarifa za viongozi wa Marekani akiwemo Rais Donald Trump mwenyewe.

Shambulio hilo, ambalo lilianzishwa mapema Jumamosi, lilikuwa sehemu ya operesheni ya kijeshi iliyopangwa kwa muda na kuelekezwa dhidi ya miundombinu ya kijeshi na maeneo ya uongozi ndani ya Iran.

Rais wa Marekani, Donald Trump, alitangaza kifo cha Khamenei kupitia mtandao wake wa kijamii na kueleza kuwa, mwendo huo ni sehemu ya mkakati mpana wa kuzuia hatari kwa usalama wa kimataifa.

Baada ya taarifa hiyo, vyombo vya habari vya serikali ya Iran viliweka bayana kwamba Khamenei mwenye umri wa miaka 86 amefariki katika mashambulizi hayo

Pia, taarifa hizo zilisema binti yake, wanafamilia wengine na mjukuu wake walifariki kutokana na shambulio hilo.
Picha na Reuters.

Mashambulizi hayo yalilenga maeneo ya uongozi na miundombinu ya kijeshi ndani ya Iran, katika kile kilichoitwa kama kampeni ya kijeshi ya pamoja na Marekani na Israel.

Mchango wa Iran katika siasa za Kiarabu na mapambano ya kikanda, pamoja na misimamo yake kuhusu programu ya nyuklia, umekuwa chanzo cha vita vya mizozo kwa miongo kadhaa.

Kufariki kwa kiongozi huyo kunazusha maswali mengi kuhusu mustakabali wa ushawishi wa nchi hiyo katika eneo la Mashariki ya Kati na uhusiano wake na mataifa mengine.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here