Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yatoa salamu za pole kifo cha Gavana mstaafu,Dkt.Idris Rashid

NA DIRAMAKINI

BODI ya Wakurugenzi, Menejimenti na Watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wametoa salamu za pole kwa wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki kufuatia msiba wa aliyekuwa Gavana wa Nne wa Benki Kuu ya Tanzania, Dkt.Idris Rashid.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 13,2026 na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Bw.Emmanuel Tutuba.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo,BoT imemkumbuka Dkt. Rashid kwa mchango wake mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa taifa na ustawi wa sekta ya fedha kwa ujumla, hususan wakati alipohudumu kama Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania kuanzia mwaka 1993 hadi 1998.

Benki Kuu imeeleza kuwa,uongozi na utumishi wake uliotukuka umeacha alama muhimu katika historia ya taasisi hiyo pamoja na taifa kwa ujumla.

Aidha,BoT imemuomba Mwenyezi Mungu awape faraja, subira na nguvu wanafamilia pamoja na wote walioguswa na msiba huo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Pia,BoT imeomba Mungu amsamehe makosa yake yote na kuipumzisha roho yake mahali pema peponi. Amina.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here