BoT yauza Dola milioni 30 za Marekani kuimarisha ukwasi wa soko la fedha za kigeni

NA DIRAMAKINI

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) imeuza jumla ya Dola za Marekani milioni 30 kupitia mnada wa ushindani katika Soko la Jumla la Fedha za Kigeni (IFEM), ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Sera ya Ushiriki wa Benki Kuu katika Soko la Fedha za Kigeni ya mwaka 2023.
Hayo ni wa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Machi 6,2026 na Kurugenzi ya Masoko ya Fedha ya BoT, ambapo mnada huo umefanyika kwa lengo la kuongeza ukwasi wa fedha za kigeni katika soko.

Katika mnada huo, kiwango cha wastani cha ubadilishaji kilichokubaliwa kilikuwa Shilingi 2,575.45 kwa Dola moja ya Marekani.

Jumla ya zabuni zilizowasilishwa na taasisi za benki zilifikia Dola milioni 39.5, huku kiasi cha Dola milioni 30 kikikubaliwa baada ya tathmini ya zabuni hizo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa, jumla ya benki 22 zilishiriki katika mnada huo, ambapo benki 18 zilifanikiwa kukidhi vigezo na zabuni zao kukubaliwa.

Aidha, viwango vya juu na vya chini vya zabuni vilivyowasilishwa vilikuwa Shilingi 2,581.00 na Shilingi 2,560.00 kwa Dola moja mtawalia.

Hata hivyo, kiwango cha juu kilichokubaliwa kilikuwa Shilingi 2,581.00 kwa Dola moja, huku kiwango cha chini kilichokubaliwa kikiwa Shilingi 2,570.00 kwa Dola moja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here