MWANZA-Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria imefanya ziara ya kutembelea na kukagua Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali lililopo Buswelu jijini Mwanza.
Kamati hiyo iliyoko chini ya Mwenyekiti wake, Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) imefanya ziara hiyo tarehe 16 Machi, 2026 na kwa lengo la kuona Maendeleo ya Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ambapo kukamilika kwake kutarahisisha upatikanaji wa Huduma za Kisheria kwa Wananchi.
Sambamba na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pia jengo hilo linatarajiwa kutumiwa na Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
Aidha, Mradi wa Ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika mkoa wa Mwanza unajengwa na Mkandarasi Suma JKT na kusimamiwa na mshauri wa majengo TBA na umefikia asilimia 74.
Tags
Bunge la Tanzania
Habari
Kamati ya Bunge
Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
















