Waziri Balozi Kombo aapishwa Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA)

DODOMA-Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) limemuapisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb.) kuwa Mbunge katika Bunge hilo leo tarehe 16 Machi 2026 katika mkutano Maalum wa Bunge la Tano la Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika kwa njia ya Mtandao (virtual platform).
Mheshimiwa Waziri Kombo ameapa kuwa` Mbunge kwa wadhifa wake wa uwaziri (ex-officio) kwa mujibu wa mujibu wa Kanuni ya 5 (4) ya Kanuni za Bunge la Afrika Mashariki ambayo inabainisha kuwa “mbunge hataweza kuketi bungeni bila kula kiapo cha utii wa Mkataba wa Uanzishwaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here