Marekani yateketeza meli tisa za kivita za Iran

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Marekani, Donald J. Trump ametangaza kuwa, jeshi la nchi yake limezizamisha na kuharibu meli tisa za kivita za Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran (Iranian Navy) katika operesheni ya kijeshi iliyoelezwa kuwa na mafanikio makubwa leo.
Rais Trump ameyasema hayo leo kupitia taarifa rasmi ambayo amebainisha kuwa, baadhi ya meli zilizolengwa zilikuwa kubwa na zenye umuhimu wa kimkakati kwa vikosi vya majini vya Iran.

Pia, amesisitiza kuwa operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi pana za kijeshi zinazoendelea dhidi ya uwezo wa baharini wa taifa hilo la Mashariki ya Kati.

“Nimeelezwa kuwa,tumeharibu na kuzizamisha meli tisa za kivita za Iran, baadhi zikiwa ni kubwa na muhimu,” amesema Rais Trump katika taarifa hiyo.

Aidha, ameongeza kuwa mashambulizi yataendelea dhidi ya meli zilizosalia, akieleza kuwa nazo pia zitalengwa hadi kuangamizwa kabisa.

Katika shambulizi tofauti, Rais huyo alidai kuwa makao makuu ya vikosi vya majini vya Iran yaliharibiwa kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo, katika kauli iliyoonekana kuwa ya kejeli, Rais Trump alihitimisha kwa kusema, “Isipokuwa hayo, jeshi la majini la Iran linaendelea kufanya vizuri.” Aidha, mpaka sasa, mamlaka za Iran hazijatoa tamko rasmi kuthibitisha au kukanusha taarifa hiyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here