Mbaroni kwa tuhuma za kuiba vifaa vya ujenzi wa barabara ya Mingoyo kwenda Mtwara

LINDI-Jeshi la Polisi mkoani Lindi limefanikiwa kuwakamata watu watatu kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vifaa vya ujenzi vinavyomilikiwa na kampuni inayojenga barabara kutoka Mingoyo kwenda Mtwara.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tukio la wizi liliripotiwa Machi 10, 2026 majira ya saa 14:00 katika eneo la Madangwa, Kata ya Sudi, Wilaya ya Lindi. Mlalamikaji, Isack Joseph maarufu Mollah (31), ambaye ni mratibu wa shughuli za Kampuni ya China Railway Construction Engineering Group Co. Ltd (CRCEG), alidai kuwa vifaa mbalimbali vikiwemo marine board, box kalavati, mbao, round pipe na nondo vyenye thamani ya shilingi milioni tano viliibwa.

Katika hatua ya upelelezi, Machi 21, 2026 majira ya saa 12:00, Jeshi la Polisi lilifanya operesheni katika Kitongoji cha Mkwajuni, Kijiji cha Zingatia, Kata ya Mnolela, Wilaya ya Lindi. Operesheni hiyo ilisaidia kukamatwa kwa watuhumiwa watatu ambao ni Abilah Mohamed Nanguka (50), mkazi wa Mnolela, Sharki Abilah Nanguka (28), mkazi wa Kijiji cha Zingatia, Joseph Tilia Filbert (47), dereva kutoka Mtwara.

Wakati wa upekuzi nyumbani kwa Abilah Mohamed Nanguka, askari walikuta vifaa vinavyodaiwa kuibwa vikiwemo vipande 24 vya marine board, round pipe 15 na nondo 15, ambavyo vilitambuliwa na mlalamikaji kuwa ni mali ya kampuni hiyo.

Watuhumiwa wote pamoja na vielelezo wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi, huku hatua nyingine za kisheria zikiendelea kuchukuliwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here