Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria awasili nchini kwa ziara ya kikazi

DAR-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Austria anayeshughulikia masuala ya kisiasa, Mheshimiwa Balozi Dkt. Hannah Liko, amewasili nchini Machi 22, 2026 kwa ziara ya kikazi ya siku tatu inayolenga kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, biashara na ushirikiano katika maeneo mbalimbali kati ya Tanzania na Austria.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dkt.Liko amepokelewa na Balozi na Mwakilishi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Vienna, Mhe. Naimi S. Aziz, pamoja na Balozi wa Austria nchini, mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Dkt. Christian Fellner.
Wakati wa ziara hiyo, Dkt. Liko anatarajiwa kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali akiwemo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe (Mb.), pamoja na viongozi kutoka wizara mbalimbali zikiwemo Ofisi ya Rais (Mipango na Uwekezaji), Wizara ya Fedha, Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara ya Viwanda na Biashara.
Aidha, anatarajiwa kutembelea Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa lengo la kuimarisha ushirikiano katika nyanja za kitaaluma na elimu ya juu. Ziara hiyo inatarajiwa kuhitimishwa Machi 25, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here