Msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026 kwa Machi 2,2026

NA DIRAMAKINI

KLABU ya Young Africans SC (Yanga SC) imeendelea kuongoza msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara msimu wa 2025/2026 baada ya kufikisha alama 29 katika michezo 11 iliyocheza hadi sasa.
Kwa mujibu wa takwimu za msimamo wa ligi, Young Africans SC imefanikiwa kushinda michezo tisa na kutoka sare miwili bila kupoteza, ikifunga mabao 27 na kuruhusu mabao mawili pekee, ikiwa na tofauti ya mabao 25.

JKT Tanzania inashika nafasi ya pili kwa alama 28 baada ya kucheza michezo 17, ikishinda saba, sare saba na kupoteza mitatu. Nafasi ya tatu inashikiliwa na Simba SC yenye alama 24 katika michezo 11, ikiwa imeshinda saba, sare tatu na kupoteza mchezo mmoja.

Pamba Jiji ipo nafasi ya nne kwa alama 24 baada ya kucheza michezo 15, huku Azam FC ikishika nafasi ya tano kwa alama 23 katika michezo 11.

Katika nafasi za katikati ya msimamo, Namungo FC, Dodoma Jiji na Mtibwa Sugar zote zimejikusanyia alama 21, zikifuatiwa na Singida Black Stars yenye alama 19.

Kwa upande wa chini ya msimamo, Mashujaa FC ipo nafasi ya 10 kwa alama 17, ikifuatiwa na TRA United yenye alama 16 na Coastal Union yenye alama 15.

Mbeya City inashika nafasi ya 13 kwa alama 13, huku Tanzania Prisons na Fountain Gate zikiwa na alama 12 kila moja katika nafasi ya 14 na 15 mtawalia. KMC FC ndiyo inayoshika mkia wa msimamo ikiwa na alama nane baada ya kucheza michezo 16.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here