Naibu Katibu Mkuu CCM Zanzibar ahimiza umoja na uimarishaji wa chama

ZANZIBAR-Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Dkt. Mohammed Said Mohammed (DIMWA) ameshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa na Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Mjini,Mohammed Ibrahim Hassanali (maarufu Raza Lee), sambamba na viongozi mbalimbali wa chama na madiwani wa baraza hilo.
Hafla hiyo ilifanyika Machi 16,2026 katika Ukumbi wa St.Beach Villa uliopo Kibweni, Mkoa wa Magharibi Unguja, Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wa ngazi mbalimbali wa CCM pamoja na madiwani wote wa Baraza la Manispaa Mjini.
Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Mohammed aliwahimiza madiwani kuendeleza misingi ya upendo, umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Aidha, aliwataka kuongeza juhudi katika kuhamasisha wanachama kushiriki kikamilifu katika shughuli za chama, pamoja na kuendeleza kampeni ya uandikishaji wa wanachama wapya.

Dkt. Mohammed pia alisisitiza umuhimu wa madiwani kusimamia na kutetea sera, misingi na mwelekeo wa CCM, akibainisha kuwa jukumu lao ni muhimu katika kuimarisha uhai wa chama na kuleta maendeleo kwa wananchi.

Akihitimisha hotuba yake, aliwakumbusha madiwani wajibu wao mkuu, ikiwa ni pamoja na kukitetea chama chao, kuitetea serikali yake, pamoja na kuwatetea wananchi waliowachagua kwa kuhakikisha wanapata huduma na maendeleo stahiki.
Kwa upande wake, Mstahiki Meya wa Baraza la Manispaa Mjini,Mohammed Ibrahim Hassanali, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya madiwani, alimpongeza Dkt. Mohammed kwa uzalendo wake na mchango wake katika kuimarisha utendaji wa CCM Zanzibar.

Vilevile, aliwataka madiwani kuendeleza umoja na ushirikiano, akisisitiza kuwa mshikamano ndiyo nguzo kuu ya kuleta maendeleo endelevu kwa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here