Naibu Waziri Maghembe aanza ziara ya kikazi nchini India

NEW DELHI-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Mhe.Dkt. Ngwaru Maghembe ameanza ziara ya kikazi nchini India ambapo pamoja na mambo mengine, atashiriki Mkutano wa Mawaziri wa Mambo ya Nje katika Jukwaa la Raisina 2026 utakaofanyika jijini New Delhi kuanzia tarehe 5 hadi 7 Machi, 2026.
Akiwa nchini humo, Mhe. Maghembe ambaye anamwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo kwenye ziara hiyo, pia atakutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa India, Mhe. Dkt. Subrahmanyam Jaishankar, Wawakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini humo pamoja na kuzungumza na Diaspora.
Mhe. Maghembe amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini India, Mhe. Anisa Mbega ambaye pamoja na Maafisa wa Wizara na Ubalozi, wametoa taarifa ya maandalizi ya ziara hiyo katika kikao kilichofanyika kwenye Ofisi za Ubalozi, New Delhi, India.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here