Naibu Waziri Maghembe azungumza na Wawakilishi wa Heshima wa Tanzania nchini Nepal, mjini Mumbai, Chennai na Kolkata

NEW DELHI-Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Dkt. Ngwaru Maghembe amekutana kwa mazungumzo na Wawakilishi wa Heshima wa Tanzania katika maeneo ya Nepal, Mumbai, Chennai na Kolkata ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi nchini India.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika jijini New Delhi hivi karibuni wamejadili umuhimu wa wawakilishi hao kushirikiana na Serikali katika kuimarisha sekta ya utalii, kilimo, elimu na biashara na uwekezaji ili kutekeleza dhana ya Diplomasia ya Uchumi.
Akizungumza, kwenye kikao kilichofanyika jijini New Delhi hivi karibuni, Mhe. Dkt. Maghembe aliwapongeza wawakilishi hao kwa kuiwakilisha Tanzania kikamilifu kwenye maeneo yao na kwamba Serikali inathamini mchango wao kwenye uwakilishi huo na itaendelea kushirikiana nao.

Kwa upande wao, wawakilishi hao Mhe. Rajesh Chaudhary wa Nepal, Mhe. Nayan Patel wa Mumbai, Mhe. Krishna Pimple wa Chennai na Mhe. Pradeep Singhania wa Kolkata wamemshukuru Mhe. Naibu Waziri kwa kukutenga muda wa kukutana nao na kwamba wataendelea kuiwakilisha Tanzania kikamilifu kwenye maeneo yao hususan katika kutangaza fursa mbalimbali zilizopo nchini ikiwemo utalii biashara na uwekezaji.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here