Wafanyakazi wanawake wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) washiriki kikamilifu maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani

DAR-Wafanyakazi wanawake wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) wameshiriki kikamilifu katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yanayoadhimishwa kila mwaka tarehe 8 Machi.
Ushiriki wao umehusisha wafanyakazi kutoka Makao Makuu ya Benki Kuu jijini Dodoma, Ofisi Ndogo za Makao Makuu zilizopo Zanzibar na Dar es Salaam, pamoja na Matawi ya Benki Kuu ya Tanzania yaliyopo Mwanza, Mbeya, Arusha na Mtwara, sambamba na Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania.
Maadhimisho ya mwaka huu yameongozwa na kauli mbiu isemayo “Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi Kufikia Dira 2050.”

Kupitia maadhimisho hayo, wanawake hao wameonesha mshikamano na uwajibikaji kwa jamii kwa kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii, ikiwemo utoaji wa misaada kwa makundi yenye uhitaji maalum katika jamii, kama sehemu ya kuendeleza utu, mshikamano na kuchangia ustawi wa jamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here