ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi amejumuika na wananchi wa makundi mbalimbali kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi katika futari aliyowaandalia Machi 5,2026 katika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil huko Kikwajuni, Wilaya ya Mjini.
"Leo nimepata fursa ya kujumuika katika futari na wananchi wa makundi mbalimbali kutoka Mkoa wa Mjini Magharibi, katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Sheikh Idris Abdul Wakil, Kikwajuni, Wilaya ya Mjini.
"Ninawashukuru wananchi wote walioshiriki katika futari hii kwa mshikamano, upendo na dua zao katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Tukio hili limeendelea kuimarisha umoja, mshikamano na maadili mema miongoni mwa jamii yetu."Naendelea kuwaombea Wazanzibari wote Ramadhani njema yenye amani, baraka na mafanikio mema kwa taifa letu,"ameeleza Rais Dkt.Mwinyi.











