NA DIRAMAKINI
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan amempangia kituo cha kazi Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Balozi Mhandisi Zena Ahmed Said amepangiwa kuwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Saudi Arabia.

