Tanzania yajivunia rekodi kulinda haki za binadamu

GENEVA-Tanzania imeihakikishia jumuiya ya kimataifa kwamba, itaendelea kuzingatia utawala wa kidemokrasia na ulinzi wa haki za binadamu.
Pia, itaendeleza mazungumzo yenye kujenga ndani ya Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC).

Msimamo huo wa serikali umekuja siku chache baada ya Kamishna Mkuu wa UNHRC, Volker Turk, kuisifu Tanzania kwa mwenendo mzuri wa kulinda haki za binadamu baada ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, kuunda Tume Huru ya Kuchunguza matukio ya ghasia katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, mwaka jana.

Akijibu hoja kutoka nchi na taasisi mbalimbali za kimataifa, mbele ya jopo la wajumbe wa UNHRC jijini Geneva, Uswisi, jana, Balozi Abdallah Possi alisema, tume hiyo huru ya Kuchunguza matukio hayo ya Oktoba 29, mwaka jana, inafanya kazi zake kwa weledi na uhuru hatua ambayo itatoa matokeo yatakayolifanya taifa kuendeleza misingi yake ya kidemokrasia, kulinda haki na uhuru.

Balozi Possi alisema, Tanzania ikiwa nchi huru yenye mamlaka kamili inao wajibu na jukumu la msingi la kuwalinda wananchi wake.

Kwa mujibu wa Balozi Possi, uamuzi wa Rais Dkt. Samia kuunda Tume hiyo ulionyesha uwazi na kuipa uhuru wa kufanya kazi zake bila kuingiliwa.

Alifafanua, kutokana na Tume kuongezewa muda hadi Aprili 3, mwaka huu, ni wazi matokeo yake yatatoa dira kuhusu mipango ya maridhiano ya kitaifa, kuelekea mageuzi ya katiba na ya kitaasisi.

Balozi Possi alisema, anaamini Tanzania itamaliza mchakato huo wa Tume ya kuchunguza matukio hayo na kuifanya nchi kuwa imara zaidi, yenye umoja zaidi na kuthibitishia dunia vurugu hazina nafasi katika utamaduni wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

WASHIRIKA

Kuhusu washirika wa kimataifa, aliwataka kuendelea kuheshimu uhuru wa Tume hiyo ya uchunguzi, kujadili masuala ya Tanzania kwa kuwa na taarifa za kweli, zilizothibitishwa na kuheshimu uhuru wa nchi.

Balozi Possi alisikitishwa na baadhi ya washirika wa kimataifa kuchagua baadhi ya matukio ya Oktoba 29, mwaka jana, jambo ambalo siyo sahihi.

Alifafanua, vurugu za mwaka jana hazikuwa za kawaida kwani kuna vituo vya polisi, mali za raia, ofisi za serikali za mitaa, miundombinu ya usafiri wa umma, nyumba za watu binafsi na biashara ziliharibiwa.

Possi aliongeza, wananchi waliotumia haki yao ya kikatiba kupiga kura walishambuliwa na kuongeza, hayo hayakuwa matukio yaliyojitokeza kwa bahati mbaya, bali kuandalowa na kupangwa mapema kwa lengo la kudhoofisha, kuharibu na kuvuruga utaratibu wa kikatiba.

Miongoni nchi zilizowasilisha hoja zao na kujibiwa kwa ufasaha na kukoshwa na majibu ni Uingereza, Sweden, Uswisi, Iralend, Ubelgiji, Norway na taasisi za Human Rights Watch na Amnesty International.

Tume ya Jaji Mohamed Chande, imekuwa ikifuatiliwa kwa karibu na taasisi za nje kwani nyingi ikiwemo UNHRC zimepongeza uamuzi huo wa kuiunda kwani unajali haki za binadamu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here