Tume ya Uchunguzi yakutana na Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa

DAR-Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imekutana na Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Parfait Onanga Anyanga.
Parfait Onanga, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi inayolenga kufanya mashauriano na Serikali pamoja na wadau mbalimbali kuhusu hali ya kisiasa nchini kufuatia matukio ya Oktoba 29, 2025.

Aidha, pamoja na mambo mengine, kikao cha Tume na Onanga kililenga kujadili namna Tume inavyotekeleza majukumu yake.
Tume hiyo ya Uchunguzi inaendelea na mahojiano na waathirika wa Matukio hayo baada ya hivi karibuni Mamlaka ya Uteuzi kuiongezea muda wa siku arobaini na mbili (42) kuanzia tarehe 20 Februari, 2026 ili Tume iweze kukamilisha kazi yake ambapo inatakiwa kukamilika na kuwasilisha Taarifa yake kabla au ifikapo tarehe 3 Aprili, 2026.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here