Tumerejesha mawasiliano Daraja la Nguva-Sanga

■Akagua na kuipongeza Serikali kuchukua hatua za haraka, Daraja hilo sasa kukamilika

DAR-Mbunge wa Jimbo la Kigamboni,Mhe. 𝗛𝗮𝗿𝗮𝗻 𝗦𝗮𝗻𝗴𝗮 ameipongeza Serikali kwa hatua za haraka za kurejesha mawasiliano katika Daraja la Nguva ambalo liliathirika na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha changamoto ya uvukaji wa wananchi kwenda upande wa pili.
Akizungumza muda mfupi baada ya kukagua maendeleo ya ukarabati huo, amsema kuwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na TANROADS wamechukua hatua za haraka kuhakikisha wananchi wanavuka na kuendelea na shughuli zao kama kawaida. Daraja hilo linaunganisha mawasiliano ya Kata za Somangila na Kimbiji katika eneo la Mwongozo na Gezauole.
“Serikali inaendelea na jitihada za kuhakikisha mawasiliano yote kwa ujumla yanarejea ambapo hadi kufikia muda huu tayari magari madogo, bajaji, pikipiki na waenda kwa miguu wameweza kuvuka kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine hii ni hatua nzuri na tunaipongeza Serikali kwa kutatua changamoto hii kwa haraka,” alisema Mhe. Sanga.

Ametumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kuzingatia taarifa na tahadhari zinazotolewa au kutangazwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa ili kuepukana na madhara yanayoweza kujitokeza hasa kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.
Kwa upande wake Meneja TANROADS mkoa wa Dar es salaam Injinia Lazeck Kyamba, amesema jitihada za kujaza kifusi ili kufikia usawa wa daraja jipya linalojengwa zinaendelea ili mawasiliano ya njia hiyo yarejee kama awali.

Ujenzi wa Daraja jipya la Nguva unaenda sambamba na Daraja la Kibugumo ambapo gharama zake ni Tsh Bilioni 9.2 fedha zilizotolewa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. 𝗦𝗮𝗺𝗶𝗮 𝗦𝘂𝗹𝘂𝗵𝘂 𝗛𝗮𝘀𝘀𝗮𝗻.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here